Maambukizi Katika Njia ya Mkojo (UTI) ni moja kati ya magonjwa ambayo
hayapewi msisitizo wa kutosha katika jamii licha ya kuwa wengi
huathirika kwa ugonjwa huu bila kujua chanzo, tiba na kinga yake.
Ugonjwa huu huanza kuathiri mirija inayopitisha mkojo, baadaye huenea
katika kibofu na figo. Mgonjwa anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo na
kupoteza maisha kama ugonjwa huu hautatibiwa mapema.
Wataalamu wa afya wanasema UTI husababishwa na vimelea ambao huingia
kupitia mirija inayosafirisha mkojo na kuutoa nje. Vimelea hawa
wanashambulia kibofu na baadaye huendelea mpaka kwenye figo. Hii ndiyo
hatua kubwa ya ugonjwa ambayo inaweza kusababisha kifo au tatizo la
kudumu.
Hawa ni vimelea wa jamii ya bakteria walio wanajulikana kwa jina la escherichia coli (E.coli).
Bakteria hawa wanapatikana katika utumbo mpana lakini husafiri
kupitia njia ya haja kubwa kwenda katika njia ya mkojo na kusababisha
maambukizi katika kibofu na figo.
0 maoni:
Post a Comment