MANCHESTER: CITY KUMVAA PILATO FA KWA KUKIUKA SHERIA ZA MADAWA HARAMU, UNITED KUMWONGEZEA FELLAINI!



ETIHADManchester City wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kukiuka Sheria za Kuzuia Matumizi ya Madawa Haramu huku Wapinzani wao Manchester United wakiripotiwa kuanzisha mchakato wa kuongeza Mkataba wa Kiungo wao Marouane Fellaini.
CITY NA PILATO WA FA
Manchester City wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kukiuka Sheria za Kuzuia Matumizi ya Madawa Haramu.
City wamepewa hadi Januari 19 kujibu Mashitaka hayo.
Imedaiwa kuwa City walishindwa kuwapa Taarifa Maafisa wanaopima Wachezaji Matumizi ya Madawa Haramu.
Kila Klabu hupaswa kujulisha Wachezaji wao watakuwa wapi kwa ajili ya kupimwa lakini City walishindwa kutoa Taarifa za Ratiba ya Mazoezi na wapi Wachezaji hao watapatikana baada ya Mazoezi ili Maafisa MANUNITED-FELLA-MOUhusika wajue wakati wote wapi watawapata wakitakiwa kupimwa.
Imedaiwa City ilishindwa mara 3 kupeleka Taarifa za waliko Wachezaji wao na ndio maana FA imewashitaki.
Kawaida kosa kama hilo huadhibiwa kwa Faini.
UNITED KUMWONGEZEA FELLAINI!
Manchester United wameripotiwa kuanzisha mchakato wa kuongeza Mkataba wa Kiungo wao Marouane Fellaini ili kumbakisha Old Trafford hadi Mwaka 2018.
Fellaini alijiunga na Man United Mwaka 2013 akitoka Everton kwa Dau la Pauni Milioni 27.5 na kusaini Mkataba wa Miaka Minne ukiwa na Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja.
Mwezi uliopita Fellaini alizomewa na Mashabiki wa Man United lakini Juzi alipiga Bao la Pili wakati Man United inaichapa Hull City 2-0 ndani ya Old Trafford katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP.
Mara baada kupachika Bao hilo, Fellaini, mwenye Miaka 29, alimkimbilia Mourinho na kumkumbatia kwa furaha na pia kuonyesha shukran kwa Meneja wake kwa kumsapoti kwenye kipindi kigumu akisakamwa na Mashabiki baada kusababisha Penati iliyowapa Everton Sare Mwezi Desemba.
Akiongea mara baada kuwafunga Hull City Juzi, Mourinho alinena: "Yeye ana moyo mgumu na amestahamili vizuri. Anajijua kwamba yeye ni Mchezaji muhimu kwangu!"
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment