ASIMAMISHWA KAZI NA KUSHTAKIWA KWA KUMDANGANYA RAIS DKT MAGUFULI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amemsimaisha kazi Mhandisi wa Ujenzi wa Mkoa Deusdedit Mshunga baada ya kubainika kuwa alimdanganya Rais Dkt Magufuli kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.
Mtaka alisema kwamba baada ya kufanya uchunguzi waligundua kuwa Rais Dkt Magufuli alidanganywa wakati akipewa maelezo ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Simiyu alipokuwa ziarani mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka kabla ya kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi na kuwahutubia wananchi wa mkoa huo.
Rais Dkt Magufuli alikataa maelezo ya gharama za ujenzi wa hospitali hiyo ambayo aliambiwa kuwa ungegharimu TZS bilioni 40 ambapo yeye aliagiza kuwa ijengwe kwa TZS bilioni 10 kama hosteli za Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) zinazojengwa na Wakala wa Taifa wa Majengo (TBA).
Tume iliyofanya uchunguzi imegundua kuwa mchoro wa ujenzi alioonyeshwa Rais Dkt Magufuli ulikuwa wa vyumba vya madarasa, vyumba vya misikiti na makanisa.
“Wataalamu wetu walimdanganya Rais juu ya uhalisia wa ramani yenyewe ambayo ilikuwa ikikadiriwa kutumia TZS bilioni 46 kwa jengo moja la wagonjwa wa nje (OPD).” alisema RC Mtaka
Aidha amesema kuwa mhandisi huyo alifanya makisio ya mchanganuo wa gharama za ujenzi kwa kuzingatia ramani ya Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambapo hata kujua gharama za ujenzi alipiga tu simu akaambiwa na yeye akawasilisha hivyo hivyo.
Amesema kuwa amemsimamisha kazi mhandisi huyo kwa kosa la kumdanganya rais na pia kutosimamia kikamilifu majukumu yake.
Aidha, Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wamemuomba radhi Rais Magufuli kwa kudanganywa na mhandisi huyo ambaye licha ya kusimamishwa na mkuu wa mkoa, katibu tawala naye amemchukulia hatua za kinidhamu. Hatua aliyochukuliwa ni kumfungulia mashataka matatu ambayo atatakiwa kuyajibu ndani ya siku 14 likiwamo la uzembe kazi.

from Blogger http://ift.tt/2kclYxN
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment