KIASI CHA FEDHA SERIKALI ILICHOOKOA KWA KUSITISHA SAFARI ZA NJE YA NCHI

Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaonyesha kuwa, serekali imeokoa kiasi cha TZS bilioni 902 kati ya Novemba 2016 hadi Novemba 2016 kutokana na kusitisha safari za nje ya nchi kwa watumishi wa serikali.
Usitishwaji huu wa safari za nje ya nchi ulitolewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli siku chache tu tangu alipoingia madarakani Novemba 5, 2015. Rais Dkt Magufuli aliyeingia na mkakati wa kubana matumizi ya serikali alisema kuwa mtumishi yeyote wa serikali anayetaka kusafiri kwenda nje ya nchi ni lazima apate kibali maalum baada ya uchunguzi juu ya safari anayoifanya kufanyika ili kuona kama ina faida kwa taifa.
Ripoti ya uchumi ya BoT inaonyesha kuwa Tanzania ilitumia kiasi cha trilioni 1.7 katika safari za nje ya nchi ikiwa ni sawa na punguzo la trilioni 1.2 ambapo kwa kipindi kama hicho Novemba 2014 hadi Novemba 2015 serikali ilitumia kiasi cha trilioni 2.64 kwa safari za nje ya nchi.
Novemba 6, 2015 Rais Dkt Magufuli alisema kuwa saafari za nje ya nchi zilikuwa zikiigharimu Tanzania fedha nyingi ambazo zingeweza kutumiwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo. Rais Magufuli alisema kuwa mtumishi yeyote wa serkali anayekwenda safari ya nje ya nchi anatakiwa kutumia gharama zake mwenyewe kama hana kibali.
Usitishwaji huu wa safari za viongozi kwa namna moja au nyingine uliathiri mashirika ya ndege yaliyokuwa yakifanya safari nje ya nchi kutokana na kupungua kwa abiria.
Mbali na kuzuia safari za nje ya nchi Rais Dkt Magufuli pia alifuta semina elekezi, alipiga marufuku kufanyia mikutano kwenye kumbi za mahoteli, kufuta sherehe za uhuru, ili kweza kukusanya fedha nyingi zaidi.

from Blogger http://ift.tt/2kb3KBL
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment