BAADA YA KUTOKA RUMANDE, T.I.D AMTEMBELEA RC MAKONDA NYUMBANI KWAKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amemualika mwanamuziki T.I.D nyumbani kwake na kufanya naye mazungumzo ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamuziki huyo alipotoka rumande.
T.I.D alitoka rumande siku tatu zilizopita kutokana na kutajwa katika kashfa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya katika orodha iliyotajwa na mkuu wa mkoa.
Haikufahamika mara moja kuwa kiongozi huyo wa mkoa alizungumza nini na mwanamuziki huyo walipokutana katika makazi yake jijini Dar es Salaa. Makonda kupitia ukutasa wake wa Instagram ameandika “Mungu wetu hajalala na siku zote anampenda amtafutae, karibu tena nyumbani T I D.”
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) na Mwanamuziki T.I.D (kulia).
Aidha, ilielezwa kuwa T.I.D alikiri kuwa aliwahi kutumia dawa hizo lakini sasa ameacha.
Licha ya kupewa dhamana na mahakama, T.I.D na wasanii wenzake wamewekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja huku wengine wakiwa chini ya uangalizi kwa miaka mitatu na kutakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi ili Polisi waweze kujiridhisha kuwa wameacha kutumia dawa hizo.
Katika wiki hii inayomalizikia watu mbalimbali wakiwemo wasanii, wanasiasa, wafanyabishara na viongozi wa dini wamehojiwa na polisi kutokana na kutuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

from Blogger http://ift.tt/2keqOj0
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment