DIWANI DEBORA SANGA AZINDUA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ WILAYA YA ILALA ILIYO CHINI YA KITUO CHA MSAADA WA SHERIA WLAC.

Watanzania wameaswa kuacha Tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa baadhi ya wanawake na watoto. 
Hayo yalisemwa na Diwani wa viti maalum (Chadema), Kata ya Segerea, Deborah Sanga Kwenye mkutano wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye shule ya msingi Tabata jijini Dar es Salaam. 
Alisema ikiwa wananchi watabaini vitendo hivyo wanapaswa kutoa taarifa mara moja katika mamlaka husika pindi wanapogundua kuwepo kwa ukatili huo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa WLAC Wigayi Kissandu, amesema kuwa ukatili huu unamadhara makubwa sana hasa kwa wanawake na watoto. Alisema kuwa vitendo vya ukatili huu wa kijinsia vmejikita zaidi katika mila na desturi na sheria mbali mbali zinazotumika ambazo ni kandamizi. 
” Ili kupunguza au kumaliza kabisa ukatili huu inapaswa kutungwa sheria mpya zitakazomaliza sheria kandamizaji dhidi ya mwanamke kama zile za mirathi na ndoa ili kuweza kumkomboa mwanamke,” alisema. 
Aidha aliongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo kwa kiasi kikubwa na kwamba katika kipindi cha Januari mwaka huu WLAC kimeshapokea kesi 150 mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia. 
Kwa upande wake Inspekta Stella Mindasi wa Dawati la Jinsia la watoto kituo cha polisi Tabata, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja, januari hadi Desemba 2016 jumla ya kesi 165 zimelipotiwa zikiwemo kubaka 24 , kulawiti 15 shambulio la kimwili 37 shambulio la aibu 6 shambulio 51, kutoa luhha yabmatusi 8 kijeruhi 15, kitelekeza familia 7, kutorosha mwanafunzi. 
Katika matukio hayo jumla ya kesi 30 zimekwishashatolewa hukumu.
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kulia) akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa na Mwanasheria WLAC, Wigayi Kisandu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. Picha na Muhidin Sufiani Mafoto Blog

from Blogger http://ift.tt/2kdV4sN
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment