Klabu ya FC itacheza dhidi ya
Mbabane Swallows Swaziland katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe
la Shirikisho Afrika (CC) utakaofanyika mwezi ujao.
Azam
FC inakutana na timu hiyo baada ya Waswaziland hao kuwatoa Orapa United
ya Botswana kwa mikwaju ya penalty 3-2 katika mchezo wa marudiano wa
raundi ya awali uliofanyika kwenye Uwanja wa Mbabane nchini Swaziland.
Mchezo huo ulilazimika kwenda hatua ya
changamoto ya mikwaju ya penalti kufuatia dakika 90 kumalizika kwa timu
hizo kwenda sare ya bao 1-1 kutokana na kila timu kushinda ugenini,
Mbabane ikishinda 1-0 nchini Botswana kabla ya jana jioni nao kupigwa
1-0.
Azam FC iliyojiwekea malengo ya kufika
hatua ya makundi ya michuano hiyo mwaka huu, itaanza kuivaa timu hiyo
nyumbani (Azam Complex) Machi 12 mwaka huu kabla kumalizia ng’we ya pili
ugenini kati ya Machi 17,18 na 19.
Mshindi wa jumla wa mchezo huo, atasonga
mbele kwa hatua ya mwisho ya mtoano (play off) na kukutana na moja kati
ya timu 16 zitakazokuwa zimetolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, mechi za kwanza zikifanyika kati ya Aprili 7, 8 na 9 na
zile za pili zikipigwa kati ya Aprili 14, 15 na 16.
0 maoni:
Post a Comment