Serikali ya Malaysia imegundua kemikali iliyotumika kumuua kaka yake kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-nam katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur mapema Februari 13 mwaka huu.
Malaysia imesema kuwa kemikali kali aina ya ‘VX Nerve Agent’ ambayo hufahamika kama silaha ya maangamizi (weapon of mass destruction) ndiyo ilitumika kumuua mtoto huyo wa kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini.
Kemikali hii ambayo ambayo ni hatari sana inaelezwa kuwa ujazo wa gramu 0.01 ambayo ni ndogo sana zaidi ya tone moja ikidondokea kwenye ngozi yako inakuua kwa kuahiribu mfumo mzima wa neva mwilini.
Video: Kaka yake Rais wa Korea Kaskazini alivyouawa uwanja wa ndege
Mtaalamu wa kemikali kutoka Malaysia amesema kuwa huenda kemikali hiyo haikuwa imechanganywa na VX ndiyo sababu wanawake wanaoonekana kama wanampaka au kumpulizia usoni Kim Jong-nam wao hawakudhurika.
Kim Jong-nam
Pia Polisi Malaysia wamesema kuwa mwanamke mmoja aliyekuwa karibu na Kim muda mfupi baada ya kushambuliwa, na yeye aliugua kutokana na kuvuta hewa yenye kemikali hiyo.
Kim Jong-nam alifariki Februari 13 muda mfupi kabla ya kufikishwa hospitali baada ya wanawake wawili kumshambulia akiwa uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Kumekuwa na tetesi kuwa Korea ya Kaskazini ndio waliohusika na kifo chake ambapo watuhumiwa watano kati ya wanane wanaoshukiwa kwa mauaji hayo ni raia wa Korea Kaskazini.
Aidha, Polisi nchini Malaysia wanachunguza ni njia gani iliyotumika kuingiza nchini humo kemikali hiyo hatari iliyopigwa marufuku.
VX Nerve Agent
from Blogger http://ift.tt/2lMxJzv
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment