Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa na taarifa za kutapeliwa wananchi kuhusu ajira za JWTZ.
Hivi karibuni kumezuka kundi la watu wanaojiita mawakala wa kutafuta vijana wa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na mara nyingi hutumia majina ya viongozi wa JWTZ kutapeli, huwataka wananchi hao kuwapa fedha ili kuweza kuwapatia nafasi hizo.
JWTZ linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa nafasi za ajira Jeshini hutangazwa kwa kufuata taratibu za ajira ambapo JKT imepewa mamlaka ya kuwachukuwa vijana kutoka uraiani kwa kutoa matangazo ya wito wa vijana wa kujitolea ambapo matangazo hayo hutolewa hadi ngazi ya wilaya, vijana hao hutakiwa kuwa na nyaraka mbali mbali zikiwemo za elimu, uraia na nyaraka nyingine kama hizo ili kukidhi vigezo vya kupatiwa mafunzo ya kijeshi.
Baada ya kumaliza mafunzo hayo wahitimu hubaki JKT kwa muda wakisubiri vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo JWTZ kutoa ajira kulingana na hitajio la vyombo hivyo. Wananchi wanatakiwa kufuata taratibu hizo ili kuepuka udanganyifu unaoweza kusababisha kutapeliwa fedha zao. Jeshi halitahusika na madai yoyote yatakayotokana na udanganyifu huo.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085
from Blogger http://ift.tt/2l6R4HS
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment