Kubenea :Chadema Tunajivunia kwa Kuokoa Bilioni 1 za Kufua Majoho ..!!!

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea amesema tangu Chadema ichukue halmashauri mbalimbali jijini hapa imefanikiwa kuokoa Sh 1.2 bilioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho ya madiwani Kinondoni na Ubungo kwa mwaka.
 
Kubenea ameyasema hayo leo wakati alipofanya mkutano wa hadhara uwanja wa Mabibo Farasi ikiwa ni ziara ya kwanza jimboni kwake tangu achaguliwe Oktoba 2015.
“Ubungo tumeokoa Sh 430 milioni zilizokuwa zinatumika kufua majoho 18 ya madiwani, Kinondoni Sh 800 milioni kwa majoho 58 na tangu Aprili mwaka jana hatujafua na hatujatoka upele,” amesema Kubenea.
Kubenea amefanya ziara hiyo na itakuwa muendelezo wa kusikiliza kero za wananchi wa Jimbo la Ubungo.

from Blogger http://ift.tt/2lZQMqO
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment