Maneno ya Cannavaro kuelekea Yanga vs Zanaco



Baada ya sare ya kufungana goli 1-1 kwenye mchezo wa marudiano kati ya Yanga dhidi ya N’gaya, Yanga imefanikiwa kufuzu kwenda raundi ya kwanza ya michuano ya mabingwa wa Afrika na itakutana na Zanaco ya Zambia katika hatua hiyo.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema, mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu anaifahamu Zanaco kuwa ni timu nzuri ambayo iliwahi kuiondosha Yanga mashindanoni wakati huo yeye ndio alikuwa anaingia kwenye kikosi hicho cha Jangwani.

“Zanaco ni timu kubwa, kipindi naingia Yanga tulishawahi kucheza nao, ni timu nzuri na ngumu na wamewahi kututoa kwenye mashindano. Naamini walimu watafanya kazi yao ili tuweze kufanya vizuri zaidi,” anasema nahodha wa Yanga ambaye alikaa benchi kwenye mchezo wa marudiano kati ya Yanga dhidi ya N’gaya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment