Mwambusi kaitaja sababu ya Yanga kushindwa kupata ushindi nyumbani dhidi ya N’gaya


Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi ametaja sababu za kikosi chake kukosa ushindi kwenye mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika wakati wanacheza nyumbani dhidi ya N’gaya na badala yake kulazimishwa sare ya kufungana 1-1.
Mwambusi amesema, kukosekana kwa baadhi ya washambuliaji nyota kwenye timu yao kulipelekea kupata matokeo ya sare nyumbani kwa sababu wachezaji waliopo walishindwa kutumia nafasi zilizopatikana.
“Kulikuwa na mabadiliko kidogo kwenye nafasi ya ushambuliaji, kuna wachezaji ambao wameshacheza na tumefanya nao mazoezi lakini bahati mbaya hawakuweza kucheza leo kwa sababu tofauti wengine wakiwa wanaumwa na wengine wana shida tofauti zilizowafanya wasicheze mchezo wa marudiano dhidi ya N’gaya,” – Juma Mwambusi.
“Katika mabadiliko tuliyoyafanya, nayo yamepunguza uwezekano wa kupata magoli kwa sababu tulicheza ugenini tukatumia krosi kupata magoli lakini leo Msuva kapiga krosi zaidi ya nne tukashindwa kuzitumia kufunga.”
“Tunamshuru Mungu mechi imemalizika salama na tumeweza kufuzu na kuvuka raundi hii, tumecheza na timu nzuri iliyojipanga na tulitarajia mechi itakuwa hivi ilivyokuwa kwa sababu tulishawafunga goli 5-1 kwao walikuja huku kucheza kwa kushambulia.”
“Nilizungumza kabla ya mchezo huu kuwa, tunahitaji kupata goli la mapema kwenye mchezo huu lakini wenzetu wakapata goli la mapema hivyo tukaendelea kurudi mchezoni. Tulipata nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini hatukuweza kuzitumia kwa sababu ya umakini mdogo wa wachezaji.”
“Tulikwenda mapumziko tukiwa tumesharudisha goli lakini bado kipindi cha pili hatukutengeneza nafasi za kutosha za kutuwezesha kupata magoli zaidi. Kikubwa tumeshavuka nawapongeza wachezaji wote kwa kupambana kuhakikisha tunavuka hii raundi, sasa akili na mawazo yetu yote ni kwenye raundi inayofata.”
Donald Ngoma na Amis Tambwe ni washambuliaji waliokosekana kwenye kikosi cha Yanga wakati kikicheza mchezo wa marudiano dhidi ya N’gaya. Tambwe alikuwepo kwenye mchezo ambao Yanga ilishinda 5-1 ugenini nay eye alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliofunga katika ushindi huo, Ngoma yeye bado anauguza majeraha na hakuwa sehemu ya wachezaji waliosafiri na timu hata kwenye mchezo wa awali.
Haruna Niyonzima pia ni mchezaji ambaye alikosekana kwenye kikosi cha Yanga kilichocheza mchezo wa marudiano lakini mchezo wa kwanza alicheza na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliochangia ushindi mkubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment