Simba hakuna kulala Zanzibar



Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’, Zanzibar

Timu ya Simba leo asubuhi imeendelea kufanya mazoezi katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya watani wao wa jadi Yanga unaotarajiwa kufanyika Jumamosi February 25, 2017 uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba wapo Unguja tangu juzi Ijumaa na wanatarajia kuondoka Visiwani Ijumaa ijayo ambapo walianza mazoezi yao jana asubuhi katika uwanjahuo wa Amaan na leo wakiendelea tena asubuhi kuanzia 3:00 hadi 5:00 ambapo kuanzia kesho Jumatatu wanatarajia kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ amesema wataendelea kufanya mazoezi hapa Unguja mpaka Ijumaa ambapo watarejea tena Dar es Salam kwa ajili ya mchezo wao siku ya Jumamosi.

“Mazoezi yanaendelea vizuri tangu juzi, tupo hapa Unguja mpaka Ijumaa, kuanzia kesho Jumatatu tutafanya mazoezi asubuhi na jioni, wapenzi wa Simba hatutowaangusha msimu huu wategemee mazuri tu kwani tunajua kuwa wana kiu ya ubingwa, sisi mechi zote ni fainali kwetu na tunaanza na hiyo ya Jumamosi kwa Yanga,” amesema Abbas.

Simba wapo katika Hoteli ya Mtoni Marine iliyopo Maruhubi Mkoa Mjini Magharibi ambapo kwa sasa wao ndio wapo kileleni mwa VPL, Ligi Kuu Vodacom baada ya kuwa na Pointi 51 kwa Mechi 22 wakifuata mabingwa watetezi Yanga wenye pointi 49 kwa mechi 21.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment