Yusuf Manji kafikishwa mahakamani na kupata dhamana ya Milioni 10 na aliemuwelekea hio dhamana ni Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwassa….
MWENYEKITI wa Yanga SC , Mh. Yussuf Manji ameachiwa kwa dhamana mchana wa leo, Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa alisimama kama wakili wake huku Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa akimdhamini.
Ahsante wana Yanga wote mlioguswa kwa hili, mliomuombea hata kumfariji mwenyekiti katika kipindi kigumu alichopitia . . Viongozi waliobaki walipambana kuhakikisha timu haitetereki na kufanya jitihada Manji arudi ofisini haraka wakalibeba tatizo kama la klabu na sio la Manji tu.
“Cannavaro na wewe Niyonzima, waambieni wachezaji wenzenu kuwa matatizo yangu yasiwahusu wala wasitetereke . . Chezeni mpira pigeni goli nyingi hicho ndio wana Yanga wanataka na itakuwa faraja kwangu pia, mi ntatoka tu na haya yote yatakwisha maana ni mambo ya kupita tu lakini mkifanya vibaya matokeo hayatofutika”
Ulikuwa ujumbe wa Manji alipotembelewa hospitali na manahodha wa timu yetu.
– Ahsante Mungu umejibu maombi ya wana Yanga .
from Blogger http://ift.tt/2llAZSN
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment