Msichana anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya Kim Jong-nam adaiwa kulipwa dola 90 sawa Tsh 200,000

Mwanamke kutoka Indonesia, aliyekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, anasema alilipwa dola 90 sawa tsh 200,000, kushiriki katika kile alichofikiri, ni kitendo cha mzaha.
Wanabalozi wa Indonesia waliokutana na Siti Aisyah, wanasema aliwaambia kuwa wanaume wawili, walionekana kama Wakorea au Wajapani, walimpa mafuta yaliofanana na yale ya mtoto kumpaka usoni mwanamme mmoja.
Mafuta hayo sasa yanafikiriwa yalikuwa na kemikali VX, moja kati ya sumu kali kabisa.
Maafisa wa polisi wa Malaysia wanasema wataanza kufagia uwanja huo wa ndege ambapo shambulio hilo lilifanyika siku 12 zilizopita ili kuchunguza sumu yoyote iliosalia.
Maafisa wa polisi wa Malaysia walivamia nyumba yake huko Kuala Lumpur mapema wiki hii ili kuchunguza mauaji hayo.
Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo ,huku washukiwa wengine saba waisakwa na polisi ikiwemo raia wanne na Korea Kaskazini.

from Blogger http://ift.tt/2lVe6FX
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment