MSUMBIJI: Mwanamke wa Kitanzania Abakwa Mpaka Kufa. Serikali Imefungwa Pasta?

Jamani, Hii inasikitisha sana tangu kuanza kusikika kwa sakata la watanzania kufurushwa uko msumbiji mengi yametokea lakini serikali yetu inaonesha kuwakandamiza watanzania kuwaonesha hawakuwa wakiish kihalali kabisa.
Okay Yote sawa mtu kwao lakini serikali ya msumbiji inafata utaratbu kuwarudsha watanzania?
Je, sisi huwa tunavunja sheria kuwarudsha kistarabu??
Maofisa wa msumbiji wamekuwa wakifanya vitendo vya kikatili ikiwemo kuwapora mali zao, pesa, na hati za kusafiria.
Sikuridhika nliamua kufunga safari kwenda mtwara kuonana na wahanga.
Katika yote kilichoniumiza nlipofanya mahojiano na mwanamke ambaye rafiki yake kutoka Morogoro alokuwa akiishi Msumbiji kubakwa na maofisa wa Msumbiji mpaka kufa akiwa anawahishwa hospital huko Msumbiji.
Tukio hilo liltokea usiku maofisa hao walivamia nyumba ya huyo mdada kisha kumbaka kwa zamu hatimaye akawa na hali mbaya hadi anakuja kupata msaada kupelekwa hospitali hali yake ilikuwa mbaya sana na kufariki dunia
Je, serikali hawajui haya? Mbona hawazungumzii lolote?
Kwanini wanaishia kuwakandamiza watanzania na kuwaonesha dunia watanzania wale hawakufata sheria?
Nimeweza kuona vibali vya wengine walofankiwa kurudi navyo vibali vya kuishi na kufanyia kazi lakini bado wamewafurusha.
Kama sheria hao wote wamevunja sheria za ukaazi?
Yupo mwingine ambaye alikuwa akiishi na mkewe na mtoto na mkewe ni mjamzito lakini alipohitaji kurudi na mkewe Tanzania maofisa wa Msumbiji walimkatalia.Je, sheria ipi inayoruhusu hayo??
Mbona wao wanarudishwa na familia zao ikiwa wamekuja nazo?
Serikali ya Tz inawaogopa Msumbiji kutetea Raia wao?
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi alizaliwa Tanzania na kusoma Tunduru na kupata mafunzo ya kijeshi hapa Tanzania.
Lakini watu hawa ambao wamesaidiwa na Tanzania wameshindwa kuagiza vikosi vyao wawarudishe kistarabu na kufata utaratbu bila kuvunja sheria?
Vipi wawafukuze kama Mbwa? Wamewafunga mahabusu bila kuwapa chakula siku tatu.
Wakawapakiza kwenye malori bila ya chakula wala mali zao.
Inasikitisha Mtanzania mwenzetu anabakwa mpaka kufa serikali haina inalosema?
Sisi mbona hawathamini watanzania na kuwaonesha dunai raia wa Kitanzania wana makosa?
Hakuna ofisa wa Msumbiji alochukuliwa sheria mpaka sasa kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ndani ya Msumbiji.
Ofisa mmoja ambaye mama yake ni mtanzania na baba yake ni Msumbiji ameambia chanzo chetu kawaida na maofisa wa Msumbiji hufanya vitendo vya kikatili kwa wageni.
Ameongeza na kusema kuwa tatizo mabalozi wa Tanzania pia sio wakali kutetea raia wao bali kuwakandamiza.
Anazidi kusema kuwa anaumia sana kuona watanzania wenzake kwa wanayofanyiwa lakini hana mamlaka ya kuweza kuzuia.
Amethibitisha pia kuwa ni kweli mwanamke huyo wa kitanzania alibakwa na maofisa wa Msumbiji wapatao sita hadi saba kwa uchunguzi wake.
Jamani tuungane tusaidie wenzetu lazima tujifunze kupendana serikali inahisi hawa watu sijui manyani sijui sio raia wao nashindwa kuelewa.

from Blogger http://ift.tt/2kFgGeC
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment