MWAKA 2017 MWEZI NA JUA KUPATWA MARA MBILI


Tarehe 26 Feburari jua litapatwa kipete. Hali hii inatokea wakati umbali kati ya mwezi na dunia unapokuwa mbali zaidi na umbali kati ya jua na dunia unapokuwa karibu kuliko siku za kawaida, mwezi utaonekana kuwa mdogo zaidi na hauwezi kufunika jua kikamilifu. Hali hii itaanzia nchini Chile na Argentina katika bara la Amerika Kusini, kupita bahari ya Atlantiki, na kuishia kusini magharibi mwa Afrika.
 
Tarehe 11 Agosti jua litapatwa kikamilifu. Hali hii inaanzia kaskazini mashariki mwa bahari ya Pasifiki, kupita Marekani na kuishia katika bahari ya Atlantiki.
 
Mjumbe wa shirika la unajimu la China Bw. Shi Zhicheng alifahamisha kuwa, mtu akikaa katika sehemu moja tu, kwa wastani anahitaji kusubiri miaka 400 hivi kuona hali ya kupatwa kikamilifu kwa jua, hivyo watu wenye hamu ya kutazama tukio hili wanaweza kutazama kupitia mtandao wa Internet au kwenda nchi nyingine.
 
Hali ya kupatwa kwa mwezi pia inastahili kutazama. Tarehe 11 Februari mwezi utaingia mahali penye kivuli kidogo tu (partial shadow) cha dunia, hivyo kwa watu wa kawaida, hawatagundua mwezi kupatwa, wataona tu mwanga wa mwezi umepungua kidogo. Tarehe 8 Agosti mwezi utapatwa kisehemu, hali hii itaonekana katika sehemu nyingi duniani ikiwemo Afrika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment