Jana kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri
kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa
na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo.
Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea.
”Siwezi
kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina
haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio
alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi
maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa
bure
”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja
“Meneja
wa zamani aliniuliza nyimbo yako inatakiwa kutumika lakini nipe idhini
yako japo ni nyimbo zangu zote lakini sikuwa na haki licha ya kuwa sauti
yangu imesikika kule, mimi nilimjibu nimeshakata tamaa na kuimba naona
muziki kwangu hauna faida na thamani bora kuwa hata mkaanga vitumbua au
maandazi kuliko kuimba
”Nilikuwa
na mpango wa kurudi kijijini nyumbani nikae mtu akihitaji show
atanikuta kijijini lakini meneja akanambia hapana, alisema nyimbo tumpe
Diamond kwa sababu itaniinua na kunipa moyo na kuniamsha upya kama mtu
aliyekufa
“Walizushaga
nimekufa na nilihisigi nimekufa kweli kutokana na hali ya maisha na
nilikuwa nimekata tamaa nikajua nimekufa kweli” Alisema Saida Karoli
Kwa
sasa Saida yupo Dar na amekuja rasmi kwa ajili ya kufanya muziki upya
kama zamani na yupo tayari kufanya kolabo na wasanii kama Ben pol, Bell
9, Diamond na Darassa.
0 maoni:
Post a Comment