Akizunguzumzia
taarifa hiyo, Mwanasheria wa mwanamuziki huyo, Amin Tenga amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa Vanessa alijisalimisha
mwenyewe katika kituo cha polisi kama alivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam wakati akitaja majina ya watuhumiwa wa dawa hizo mapema
mwezi uliopita.
Vanessa
ni miongoni mwa watu waliotajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za
kulevya, lakini hakuweza kuripoti kwa wakati sababu alikuwa nchini
Afrika Kusini kikazi.
Baada
ya kujisalimisha, Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi nyumbani kwake
kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi
zaidi.
Jeshi la Polisi hadi sasa halijatoa taarifa kuhusu tukio hilo na kama walikuta ushahidi wowote nyumbani kwa mwanamuziki huyo.
0 maoni:
Post a Comment