Mwanamke aliyenusurika Kuuawa Kisa Mumewe Ni Jambazi Sugu Kupewa Ulinzi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla ameagiza kupewa ulinzi mwanamke anayedai kutaka kuuawa na wananchi kwa kuwa mumewe ni jambazi sugu.
Makalla alitoa agizo hilo jana baada ya mwanamke huyo, Mkazi wa Kata ya Iyela jijini humo, Atupakile Frank (32) ‘kuvamia’ kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa akiwa na watoto wanne, akiiomba Serikali imhifadhili na kumlinda.
Makalla alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika kuhakikisha familia hiyo inakuwa katika mikono salama na kumtaka mwanamke huyo kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kufichua alikokimbilia mume wake anayetuhumiwa kwa uhalifu.
Mkuu wa wilaya hiyo, alisema Serikali itafuatilia sababu za wananchi kumfukuza mwanamke huyo katika makazi yake na kumtaka mlalamikaji kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi.
ANGALIA VIDEO CHIDEO

from Blogger http://ift.tt/2lUdsIN
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment