Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye anapenda sana magari na katika magari hayo yeye anapendelea zaidi magari makubwa makubwa.
Akiongea kwenye kipindi cha KIKAANGONI , Mzee wa Upako alisema kuwa hapendi kabisa “vigari vidogo vidogo” na kudai kuna gari hawezi kabisa kuendesha.
“Mimi napenda sana magari mazuri mazuri kwa sasa natumia gari aina ya V8 Land Cruiser ile kubwa kabisa. Napenda gari kubwa Benz, BMW, Land Cruiser zile kubwa kabisa hizi ndiyo gari nazopenda sana kwa hiyo hizo zingine inategemea naweza kuendesha maana wakati mwingine unaangalia na hali kama hali ikiwa mbaya basi unatembelea hata bajaji ila mimi napenda magari makubwa” alisisitiza Mzee wa Upako
Pia hakusita kutaja aina ya gari ambayo hawezi kuendesha kuwa ni Vits “Kuendesha Vits hata siku moja siwezi, hivi vigari vidogo vidogo hivi hapana sitaki, yaani sipendi”
from Blogger http://ift.tt/2lm5ecf
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment