ORODHA YA ASKARI 12 WALIOSIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Jeshi la Polisi nchini limewasimamisha kazi watumishi wake 12 kufuatia tuhuma zinazowakabili za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Tuhuma hizo zilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kueleza kuwa alifanya uchunguzi na kubaini watu wanaokwamisha mikakati ya kutokomeza dawa hizo zinazomaliza nguvu kazi ya taifa.

Akizungumza wakati wa kutoka maagizo hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejidhatiti katika kumaliza biashara ya dawa za kulevya na Jeshi la Polisi ni moja ya vyombo vinavyotumika kumaliza biashara hiyo. Kufuatia hali hiyo, Askari Polisi kutuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya si tuhuma ndogo.

Kuhusik kwa Askari katika sakata hili kunafanya vita ya kumaliza dawa hizi kuwa ngumu kwani wananchi hawatakuwa tayari kutupa ushirikiano kwa taarifa wanazozijua, hawatatuamini na hata wahalifu hawatatuogopa, alisema IGP Mangu.

IGP Mangu alisema kuwa wamewasimamisha kazi kupisha uchunguzi na watakapobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Wafuatao wamesimashwa kazi na Mkuu wa Jeshi la Polisi kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma za kujihusisha na dawa za kuelvya.

  1. PF 14473 SACP Christopher Fuime
  2. PF. 17041 INSP Jacob Hashimu Swai
  3. D3499 D/SGT Steven Apelesi Ndasha
  4. E 8431 D/SGT Mohamedi Juma Haima
  5. E/ 5204 D/SGT Steven John Shaga
  6. E. 5860 D/CPL Dotto Steven Mwandambo
  7. E. 1090 D/CPL Tausen Lameck Mwambalangani
  8. E. 9652 D/CPL Benatus Simon Luhaza
  9. D 8278 D/CPL James Salala
  10. E 9503 D/CPL Noel Masheula Mwalukuta
  11. WP 5103 D/C Gloria Mallya Massawe
  12. F 5885 D/C Fadhili Ndahani Mazengo

from Blogger http://ift.tt/2lb0DFR
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment