WASANII WALIOITWA KUHOJIWA NA MAKONDA WALALA RUMANDE

Juzi Alhamis Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda alitaja majina ya watu kadhaa yakihusisha askari wa Jeshi la Polisi pamoja na wasanii wa muziki na filamu nchini. Watu hawa ambao majina yao yalitwajwa katika mkutano ambao Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alifanya na waandishi wa habari, walitakiwa wafike Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es salaam siku ya jana bila kukosa kwa ajili ya mahojiano.
Mwanamuziki TID alipokuwa akiwasili kituo cha polisi jana kuitikia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Jana kupitia televisheni mbalimbali nchini tuliwashuhudia wengi kati ya wasanii hao waliotajwa wakiwasili katika kituo hiko kutii agizo hilo ambapo baada ya mahojiano nao, Mh. Mkuu wa Mkoa aliongeza majina mengine kwenye idadi hiyo, akiwemo mwanamuziki Vanessa Mdee (Vee Money).
Mategemeo ya wengi ni kwamba baada ya kumalizika kwa mahojiano haya, wale walioonekana hawana hatia yoyote wangeachiwa huru na si kulala rumande ikiwa haijathibitishwa hatia za tuhuma dhidi yao.
Muigizaji Wema Sepetu alipokuwa akiwasili kituo cha polisi jana kuitikia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Awali, watu hawa walitakiwa kufika kituoni ili kujibu tuhuma zinazowakabili kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya au usambazaji wake.

from Blogger http://ift.tt/2laS7aK
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment