Wahenga walisema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Pengine msemo huo unatosha kuelezea tukio hili ambalo limewaacha wengi vinywa wazi baada ya picha za kuku akifanya mazoezi na polisi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Picha hizo zinawaonyesha askari wakiwa wamejipanga katika mistari mitatu huku wakifanya mazoezi ya kunyanyua na kushusha mguu. Katika msatari wa katikati kuna nafasi ya askari mmoja ambapo amesimama kuku huyo huku naye akifanya kama wafanyavyo askari hao wengine.
Majeshi mbalimbali dunia hutumia wanyama katika shughuli zao za ulinzi ambapo wanyama maarufu ambao hutumika zaidi ni Mbwa, Farasi na Panya.
Mbwa wa Polisi akikagua mizigo kubaini kama kuna kitu chochote hatarishi.
Mbwa hutumika zaidi kwenye kumkamata adui, kutegua mabomu na kwenye ukaguzi mfano kubaini wenye dawa za kulevya, kwa upande wa farasi, hutumika zaidi kwa kufukuzua adui sehemu ambapo ingekuwa vigumu kutumia gari au pikipiki, na panya hutumika kwenye shughuli za kitafiti na pia na uteguaji mabomu.
Kuku huyu anaonekana kuwa amefunzwa na ndio sababu anaweza kufuatisha kama wafanyavyo askari hao. Baadhi ya mataifa pia hutumia ndege (mwewe au njiwa) kwa ajili ya kunyakuwa vitu angani kama vile ndege ndogo zisizo na rubani (drones).
Ndege akinyakuwa drone akiwa angani
from Blogger http://ift.tt/2lkKZf4
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment