PICHA: WATU 12 MASHUHURI WANAOSAFIRI KWA NDEGE BINAFSI TU

Wengi wetu, tukisafiri kwa mara moja tu kwenye daraja la kwanza basi tutafululiza Snapchat na Instagram mpaka watu washike adabu zao. Kwa watu wengi mashuhuri duniani, kumiliki ndege binafsi ndio lengo kuu kabisa kuashiria mafanikio. Wanaweza kusafiri dunia nzima yalipo majumba yao ya kifahari bila bugudha yoyote, muda wowote wanaotaka, wakiepuka kusafiri na watu wa kawaida.
Bila ubishi watu mashuhuri pia wanapenda kulinganisha ndege zao. Ukiwa nayo kubwa zaidi ndio bora zaidi. Inakwenda kwa kasi gani? Watu wangapi wanaweza kusafiri kwenye ndege hiyo kwa wakati mmoja? Au, unamiliki ndege ngapi? Wengine wana ndege nyingi ambazo wakizipaki huonekana kama kapaki magari tu, na kwao wanaona kawaida, sio kitu kikubwa kiasi hicho!
Hawa ni mastaa ambao safari zao huzifanya kwa ndege binafsi tu, tena zile wanazozimiliki wenyewe.

1. John Travolta

Yawezekana Travolta ndio mtu mashuhuri na pia rubani mwenye mafanikio makubwa sana. Anamiliki ndege saba ikiwemo Boeing 707 yenye uwezo wa kubeba watu 219, Bombardier Challenger 601 inayochukua watu 19, Boeing 727 inayobeba watu 189 na ndege tatu za kifahari aina ya Gulfstream.
2. Tom Cruise
Image result for the g4 plane
Anamiliki ndege binafsi ya kifahari inayoitwa G4 ambayo ni maarufu sana katika ulimwengu wa ndege binafsi. Inauzwa shilingi bilioni 80.85

3. Mark Cuban

Cuban anamiliki ndege kubwa aina ya Boeing inayouzwa bilioni 323.6, lakini pesa hii ni chenji kidogo tu kwa bilionea huyu, na hii ni moja tu kati ya ndege zake.

4. Tiger Woods

Mcheza gofu huyu maarufu huwa anakwenda uwanjani kutumia ndege yake aina ya Gulfstream G550, inayouzwa bilioni 119.

5. Donald Trump

Trump anamiliki ndege binafsi aina ya Boeing 757 inayouzwa bilioni 215. Baada kuwa Rais wa Marekani, Trump haruhusiwi tena kutumia ndege yake binafsi kwakuwa kufanya hivyo itakuwa ni kwenda kinyume na protokali za ulinzi wa nchi hiyo.

6. Harrison Ford

Ford mwenyewe ni rubani,huwa anairusha mwenyewe ndege yake aina ya Cessna 680 Sovereign, ambayo ni moja kati ya ndege zake nane. Ndege hii inayouzwa shilingi bilioni 40.4 in uwezo wa kubeba watu 12.

7. Jim Carrey

Mchekeshaji huyu anahusudu sana kusafiri kwa ndege yake hii aina ya Gulfstream V, inayouzwa shilingi bilioni 132.5
8. Rais wa Marekani
Ndege anayotumia Rais wa Marekani imepewa jina la Air Force One, zimekuwa zikibadilisha kwa miaka mingi ila kwa sasa ni ndege aina ya Boeing 747-200B inayouzwa shilingi bilioni 876.

9. Roman Abramovich

Image result for abramovich private jet interior
Huyu ni bilionea wa Kirusi na mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya nchini Uingereza, anamiliki ndege binafsi aina ya Boeing 767 iliyoongezwa vitu anavyovitaka yeye ndani (customized) aliyoipa jina la “The Bandit (jambazi).”
10-12. Oprah, Celine Dion, and Steven Spielberg
Watu hawa waliopo katika kiwango cha ufalme na umalkia katika soko la burudani duniani, kila mmoja anamiliki ndege aina ya Bombardier Global Express XRS, inayouzwa shilingi bilioni 94 kila moja.

from Blogger http://ift.tt/2keVTSf
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment