MASWALI 7 KWA WAZIRI WA FEDHA KUHUSU UCHUMI WA NCHI

Wabunge wengi wameoneshwa kuwa na wasiwasi na muelekeo wa uchumi wa nchi kwa sasa. Hili lilikuwa wazi wakati wa mjadala wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kutokana na hoja saba walizozielekeza kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango wakiitaka serikali kuhakikisha inawapatia wananchi nafuu ya kiuchumi tofauti na ilivyo sasa.

Maswali hayo ni:

  1. Hali mbaya ya deni la Taifa
  2. Kutopelekwa kwa fedha za miradi
  3. Kukosekana kwa safari za nje
  4. Kasi kubwa ya kufungwa kwa biashara nchini
  5. Athari za makato makubwa ya miamala ya simu
  6. Fedha kutoweka mitaani
  7. Utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kama ilivyopitishwa na Bunge Juni 2016

Waziri Mpango alijibu baadhi ya hoja hizo. Amesenga msingi mkubwa wa kuzuia safari za nje ni kubana matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zitakazookolewa ziwanufaishe wananchi.

Kuhusu kufungwa kwa biashara, Naibu Waziri amesema kuwa kuzibwa kwa mianya ya kukwepa kodi zikiwemo za wafanyabiashara za maduka ndio sababu ya wale waliokuwa hawalipi kodi kufunga biashara zao, hata hivyo alisema biashara zilizofungwa ni 4,183 wakati biashara mpya zilizofunguliwa ni 139,554, hivyo hakuna athari yoyote iliyojitokeza.

from Blogger http://ift.tt/2keTAyq
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment