Rais wa Uganda kuzuru Tanzania kwa siku mbili kuanzia leo


Rais wa Uganda Yoweri Museveni 
 
Rais wa jamuhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni anatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia leo Jumamosi lengo kuu likiwa kuimarisha mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Rais Museveni anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli ambapo pia atatembelea viwanda vya kampuni ya Said Salim Bakhresa ambaye amewekeza pia nchini Uganda.
Aidha rais Museveni pia atatembelea bandari ya Dar es salaam kujionea utendaji kazi unavyoendelea katika bandari hiyo baada ya hivi sasa asilimia kubwa ya mizigo ya nchi hiyo kusafirishiwa kupitia bandari ya Mombasa tofauti na hapo awali ambapo bandari ya Tanzania ndio ilikuwa inasafirisha asilimia kubwa ya mizigo hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari waziri wa mambo ya kigeni na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania Balozi Dkt Augustine Mahiga amesema mambo mengine ambayo yataongelewa katika ziara hiyo ya siku mbili ni hatua ambazo zimepigwa katika ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta gafi kutoka Hoima katika ziwa Albert Uganda hadi bandari ya Tanga.
Bomba hilo ambalo litakuwa na urefu wa km 1442 na kwa upande wa Tanzania peke yake litakuwa na urefu wa Km 1147, na baada ya kufika kwenye bandari ya Tanga ndipo yatasambazwa sehemu mbalimbali duniani na ujenzi wa bomba hilo unatarajia kutoa ajira kwa watanzania wasiopungua elfu kumi.

CHANZO IDHAA YA KISWAHILI YA UFARANSA.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment