Nay wa Mitego amesema ni tofauti na alivyofikiria kwani baada ya kupokea simu hiyo ya katibu mtendaji wa baraza hilo amemsifia kwa mashairi na maudhui yaliyopo kwenye wimbo wake huo mpya aliouachia rasmi leo Feb 16 kwenye vituo na mtandao.
Nay wa mitego ameyazungumza hayo alipokua kwenye mahojiano na XXL ya CloudsFM na amesema hii kwake ni mara ya kwanza kupigiwa simu na kusifiwa na BASATA >>> ‘Miongoni mwa watu walionipigia simu baada ya kuusikia wimbo huu ni Katibu wa Basata kasema una maudhui mazuri,hii ni mara yangu ya kwanza kusifiwa na Basata’
0 maoni:
Post a Comment