Shirika la
reli la Uingereza linaloundwa na makampuni mbalimbali ya reli limetoa
ripoti ya maendeleo ya reli ikisema katika siku zijazo kampuni hiyo
itaboresha miundombinu na vifaa vya reli, na kutumia treni mpya zisizo
na dereva, ili kuinua ufanisi na kukidhi mahitaji ya usafiri wa treni
yanayoongezeka siku hadi siku.
Shirika hilo limetoa mapendekezo mbalimbali ya kuendeleza teknolojia
za usafiri wa treni, ikiwemo kutumia treni "zenye akili" ambazo
zinawasiliana kupitia sensa na vyombo vya kutoa ishara, ili kujiendesha
zenyewe na kuepuka kugongana.
Treni zisizo na dereva zikitumiwa kwa wingi, si kama tu usafiri huo
utakuwa na ufanisi mkubwa zaidi, bali pia hali ya kuchelewa kwa treni
haitatokea mara kwa mara. Aidha, gharama ya nguvu kazi ni ya juu nchini
Uingereza, hivyo treni zisizo na dereva zikitumiwa, inakadiriwa kwamba
kwa ujumla makampuni ya reli ya Uingereza yatapunguza gharama ya nguvu
kazi kwa pauni milioni 340 kila mwaka.
Ripoti hiyo pia inasema serikali ya Uingereza imetunga mpango wa
uwekezaji wenye thamani ya pauni milioni 45 ili kuendeleza reli
zinazotumia teknolojia mpya. Teknolojia ya upashanaji ishara itafanyiwa
majaribio, ambayo ni hatua ya kwanza ya kuendeleza treni zisizo na
dereva.
0 maoni:
Post a Comment