Wataendelea kutulaza ndani - Billnass




Mwanamuziki wa Hip hop kutoka lebo ya (LFLG) Billnass anayefanya poa na ngoma yake 'Mazoea' amesema yeye hakwenda kituo cha polisi kuwaangalia mabosi zake waliokuwa wametuhumiwa kujishughulisha na dawa ya kulevya ili wajifunze maisha.
Rapa Country Boy (kushoto) Billnas (katikakati) wakiwa na meneja wao Pet Man katika kipindi cha Friday Night Live.
Katika kipindi cha Friday Night Live (FNL) cha EATV Billnass alisema katika maisha aliyoishi yeye suala la kwenda ndani ni jambo la kawaida sana hivyo kutokwenda kuwaona maboss zake ambao ni Pet Man na Mchafu Chakoma kipindi wamepatwa na matatizo si jambo la msingi na kusema yeye hawezi kuhama label yake kwa ajili ya maboss zake wamehusishwa na dawa za kulevya.
"Siwezi kuhama label eti sababu kuna watu wamelala ndani, hata baba na mama yangu mimi pia walishakaa ndani, kwa mazingira niliyokulia mtu kuwekwa ndani jambo la kawaida na wataendelea kutuweka ndani".- Alisisitiza Billnass 
Aidha Billnass ameongeza kuwa Mwana FA kumfunika katika wimbo wake wa Mazoea aliomshirikisha ni heshima sana kwakwe kwa kuwa msanii huyo ni mkongwe kwenye kiwanda cha muziki pamoja na hayo amedai hakuna Dj ambaye anaweza kuminya kipande alichokiimba yeye na kukicheza cha mwana FA peke yake kwani wote wameutendea haki wimbo huo.
Pia msanii huyo amekanusha kuwahi kuwa na mahusiano na msanii Linnah Sanga ambaye ukaribu wao ulifanya watu wengi kuhisi kwamba ni wapenzi.
"She was good friend of mine, hakuwai kuwa mpenzi wangu kuhusu mimba tutajua mtoto akizaliwa maana huwezi kujua, yule mtoto ni wa nani inawezekana atakua wangu au laa!.-  Alisema Billnass akiwa anacheka
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment