Ikiwa leo ni siku ambayo ilikuwa inasubiriliwa kwa hamu kubwa sana kwa mashabiki wa Simba na Yanga kutokana na klabu hizo kukutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara, katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga , Charles Boniface Mkwasa
Klabu ya Yanga imefunguka na kumuomba mwamuzi wa leo Mathew Akrama kutoka Mwanza kuchezesha mchezo huo kwa kufuata utaratibu.
Klabu ya Yanga imeanza kuonyesha wasiwasi dhidi ya waamuzi wa mechi hiyo na kusema wapinzani wao ambao ni Simba tayari walikuwa na majina ya waamuzi hao kabla hata ya kutangazwa na Kamati ya Maamuzi.
"Namasikitiko kwamba haya majina ya waamuzi yameanza kutajwa kutoka jana (Juzi) nafikiri wapinzani wetu walikuwa nayo mapema toka jana (juzi) na yamekuwa yakitajwa tajwa kwenye mitandao, sisi kama Yanga tunamuomba mwamuzi achezeshe kwa mujibu wa kanuni 17 na kusiwe na aina yoyote ya tofauti yenye kuonyesha kuna upendeleo wowote, niwasihi wana Yanga wawe watulivu na wamemakini maana hata watu wa usalama wamekiri kabisa kama ikitokea mwamuzi atakwenda tofauti na taratibu na sheria basi atachukulia na kufunguliwa mashitaka pale pale" amesema  Katibu Mkuu wa Yanga , Charles Boniface Mkwasa
Mbali na hilo  Charles Boniface Mkwasa alisema kuwa anatambua kipindi cha nyuma kulikuwa na matatizo dhidi ya mwamuzi huyo lakini wao wanasema yote hayo wameyaweka pembeni na kusema wanachotaka saizi ni kupata fair play. 
"Sisi tunaheshimu na tunamweshimu mwamuzi huyo ila tunamuomba tu achezeshe vizuri tunajua hapo nyuma kulikuwa na matatizo, kuna mechi zingine alichezesha ndivyo sivyo lakini yote hayo sisi tumeyaweka pembeni, tunachotaka saizi tupate 'fair play' timu ishinde kwa uwezo wake kuliko kuwa na mbeleko ya kubeba timu nyingine kwa ajili ya faida ya timu nyingine" alisisitiza  Charles Boniface Mkwasa
Pia Mkwasa alisema kama yakitokea mambo ya ajabu ajabu kama hayo wanaweza kusababisha usalama wa Uwanja hivyo amewataka kuwa makini wafuate sheria 17 za mchezo ili mshindi apatikane kiuhalali.