Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye aongoza timu yake katika operesheni maalumu ya kufanya msako mkali wa wauzaji wa kazi za wasanii bila vibali vya Bodi ya filamu ya Tanzania.
Waziri huyo amevamia maduka yanayouza CD FEKI pamoja na ofisi ambayo inajihusisha na kurudufu kazi za wasanii kutoka ndani na nje ya nchini.
Hii ni ziara ya Pili kuifanya Kariakoo. Ziara ya kwanza ya kushitukiza aliifanya July 15, 2016 ambapo aliwataka wauzaji wa CD kote nchini kufuata sheria ya kuuza CD zenye stika huku akisema mtu yoyote ambaye atakutwa na CD ambayo haina stika mnunuaji na muuzaji wote watakamatwa.
Operesheni hizi zinafanywa kwa lengo la kutokomeza uharamia wa bidhaa za filamu na muziki kwa kuokoa pato la TAIFA.
Amesema Seikali itawachukulia hatua za kisheria ikiweemo kuwafutia leseni wauzaji na wasambazaji wa filamu nchini ambao wamekuwa wakiuza bidhaa hizo bila vibali kutoka kutoka mamlaka husika jambo ambalo likiikosesha serikali mapato pamoja na kuchangia momonyoko wa maadili katika jamii.
CHEKA KIDOGO NA HUYU JAMA ASIEJUA KUCHEZA KWAITO
from Blogger http://ift.tt/2lqMTdr
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment