Kutokana na mabadiliko ya mwongozo wa ufanyaji wa Tamasha la Tuzo za Gospo Awards kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) uongozi wa GospoMedia na kamati ya maandalizi ya tuzo za Gospo Awards tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kupelekwa mbele kwa sherehe za ugawaji wa tuzo hizo ambazo zilibidi zifanyike tarehe 30 April 2017 katika kanisa la CCC Upanga mpaka utaratibu mpya utakapokuwa tayari.
Katika kipindi hiki yafuatayo yatazingatiwa;
1/mfumo wa upigaji kura ambao ulibidi ufungwe tarehe 30 Aprili 2017 utasitisitiswa kwa muda (utasitishwa jumatatu saa mbili asubuhi) na kufunguliwa tena wiki moja kabla ya tukio rasmi la ugawaji wa tuzo kufanyika mara baada ya mabadiliko ya mwongozo kutoka BASATA kukamilika.
2/Taarifa kamili na maelezo zaidi yatatolewa siku ya jumatano, tarehe 26 Aprili 2017, Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na uongozi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 755 038 159 au +255 679 433 323
0 maoni:
Post a Comment