Zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu rapa Ibrahim Mussa aka Roma Mkatoliki na wenzake watatu, Moni, Imma na Bin Laden, walipotekwa wakiwa kwenye Studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki, habari mpya ni kwamba studio hiyo imefungwa na haifanyi kazi kwa sasa.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii Mkurugenzi wa Studio hiyo, J Murder amedai studio hiyo itafunguliwa baada ya mambo kukaa sawa.
“Ni kweli Studio kwa sasa haifanyi kazi kwa sababu watu bado hawajakaa sawa, wanahitaji kupunzika kwanza,” alisema Murder. “Mimi nadhani kwa sasa afya ya vijana wetu ndio kipaumbele cha kwanza, mambo yakitulia kila kitu kitakuwa wazi,”
Roma anaendelea kuuguza majeraha na bado hajarudi kwenye ubora wake, huku polisi wakiendelea na uchunguzi kwenye sakata hilo la utekwaji.
0 maoni:
Post a Comment