Asikuambie mtu, Haji Manara wa Simba SC na mkuu wa zamani wa kitengo cha habari na mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro ni marafiki.
Baada ya Manara kupewa adhabu ya kufungiwa kutokujihusisha na soka na kamati ya maadili ya TFF, Jerry Muro ametoa neno kwa mashabiki na wadau wa soka kupitia mtandao wa Instagram.
Muro ameandika, “Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa, haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara.”
Msemaji huyo wa zamani wa Yanga na yeye alifungiwa mwezi Julai mwaka jana na kamati hiyo ya TFF kutojihusisha na mchezo huo kwa kipindi cha mwaka mmoja huku pia akitakiwa kutoa faini ya shilingi milioni tatu.
0 maoni:
Post a Comment