Wikiendi hii yalifanyika mashindano ya riadha ya London Marathon, ambako Mtanzania Alphonce Simbu aliibuka mshindi wa tano. Prince William na mkewe Catherine Elizabeth (Kate) ni baadhi ya wageni waliohudhuria katika mashindano hayo.
Katika mbio hizo Daniel Wanjiru kutoka Kenya aliibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume baada ya kukimbia kwa muda wa masaa 2:05:48 na upande wa wanawake Mary Keitany naye kutoka Kenya alishinda baada ya kukimbia kwa muda wa masaa 2.17.01.
Hizi ni baadhi ya picha za Prince William na mkewe Kate Middleton katika mashindano hayo.
0 maoni:
Post a Comment