Kupitia mtandao wa Instagram, hitmaker huyo wa Wapo ameonekana kuguswa na maneno aliyomfungukia mzazi mwenzake na sasa ameahidi kupeleka fedha za matumizi kwa mtoto wake huyo.
“Si kwa kichambo kile jamaniiiiii huh🏃🏿! Jamani inatosha basiii Povuuu. Nitapeleka Matumiziiiii😂😂😂. Nawapenda sana awa Watoto Wanguu😄. Wasiopeleka Matumizi ya Watoto😂😂 #Wapo,” ameandika Nay katika mtandao huo.
Chanzo cha Skyner kuamua kumshushia kichambo hiko mzazi mwenzake [Nay] ilitokana na rapper huyo kuweka picha kwenye Instagram ya mwanae na kuandika, “My lovely Daughter #Munie Mungu akulinde, akuepushe na Mijanaume Mijangili. Maana hii Bastola nimenunua kwa ajili yao wakianza tu ujinga wao, na vunja miguu yao.! Happy birthday to you my Munie🎂🎂.”
Hapo ndipo muigizaji huyo alipoamua kutumia fursa hiyo kupitia mtandao huo huo kwa kuandika ujumbe mrefu uliosomeka:
Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya Watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. Nimevumilia sana it’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa. Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake.
Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”
Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness
0 maoni:
Post a Comment