Afrika Kusini yakubali kuisaidia Tanzania kiuchumi

mediaRais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akipeana mikono na rais wa Tanzania John Magufuli baada ya kushuhidia utiwaji wa saini wa mikataba ya ushirikiano. 
 
Rais wa Tanzania John Pombe Magufulu amemuomba rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kutumia uwepo wake kwenye jumuiya ya nchi za BRICS kuisaidia ipate mkopo wa masharti nafuu kutoka kwenye nchi wanachama.

Rais Magufuli amesema nchi ya Afrika Kusini imeendelea kiviwanda na kiuchumi na inaweza kuwa sehemu ya kuisaidia Tanzania inapoelekea kuwa nchi ya viwanda kwa kuzungumza na nchi wanachama za BRICS, akisema nchi yake ilikuwa chachu ya harakati za ukombozi wa taifa la Afrika Kusini.
Kwa upande wake rais Zuma mbali na kuishukuru Tanzania kwa mchango wake wakati wa harakati za ukombozi kwenye nchi za kusini mwa Afrika, amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na usalama barani Afrika.
Viongozi hawa wawili wamekubaliana pia kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi zao ili kurahisisha ufanyaji wa biashara kati ya raia wa Afrika Kusini na wale wa Tanzania.
Afrika Kusini pia imekubali kuisaidia Tanzania katika kukamilisha ujenzi wa reli ya kati ya kisasa.
Rais Jacob Zuma anatarajia kumaliza ziara yake hii leo nchini Tanzania ambapo hapo jana yeye pamoja na mwenyeji wake walishuhudia utiaji saini wa mikataba kadhaa ya ushirikiano kwenye ikulu ya Dar es Salaam.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment