Mashambulizi ya kimtandao yaathiri mataifa mia moja dunianiPixabay
Mashambulizi
ya kimtandao kwa kutumia vifaa vya udukuzi vinavyoaminika kutengenezwa
na idara ya usalama wa taifa la Marekani NSA yameathiri maelfu ya
kompyuta za takribani mataifa mia moja.
Watafiti
wenye mbinu za kiusalama za kukabiliana na athari hizo wamethibitisha
athari zaidi ya elfu hamsini kwa mataifa 99 ikiwemo Urusi Ukraine na
Taiwan mlengwa nambari moja.
Wizara ya mambo ya ndani nchini Urusi imesema baadhi ya kompyuta zake zimeshambuliwa na virusi.
Msemaji wa wizara hiyo Irina Volk ameliambia shirika la habari la Urusi kuwa imerekodi mashambulizi ya kimtandao katika kompyuta za wizara zinazoendeshwa kwa mfumo wa Window.
Hata hivyo amedai hatua zimechukuliwa kwa lengo la kuangamiza na kudhibiti virusi hivyo.

0 maoni:
Post a Comment