Mbeya City imesema haitaki
kuwa ngazi ya Yanga kutwaa ubingwa hivyo watahakikisha hawapotezi mechi
ya leo itakayopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Katika
mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya, timu hiyo iliibuka kidedea dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi
Kuu, Yanga.
Kocha wa Mbeya City Kinna Phiri alisema mchezo wao dhidi ya Yanga utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao hao kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao, lakini hawatakubali kuwa ngazi. “Tumefanya maandalizi mazuri na tumerudi kutoka Sumbawanga, ambako tuliweka kambi ya siku tano na kucheza michezo minne ya kirafiki, ambayo tulishinda yote,” alisema Phiri.

0 maoni:
Post a Comment