Miriam amefunguka hayo katika kipindi cha Gospel Trending na kuongeza kuwa si vibaya kwa kama waimbaji wa Gospel watawaita waimbaji wa secular waje kumuimbia Mungu kama wakipenda lakini sio wao kwenda kuimba nyimbo za kidunia.
“Unapomshirikisha mtu ambaye anaimba secular wakati wewe unaimba Gospel hata kama wote tunaimba muziki lakini tunatofautiana imani,kwangu mimi hiyo sahihi lakini
kumuita mwanamuziki wa secular tukamuimbie Mungu sio shida kama atakubali kwa sababu sisi tumeitwa kuwahubiria watu” alifunguka Miriam
Hata hivyo Miriam amedai kuwa kuna mazingira yanayoweza kuwafanya waimbaji wa Gospo na waimbaji wa kidunia (secular) kufanya kazi pamoja kwa mfano kuimba nyimbo kwa ajili ya kugusa jamii au nyimbo za kuimbia taifa na si vinginevyo.
Kwa namna moja au nyingine hatuwezi kujua Miriam alikuwa ana mlenga mwimbaji au waimbaji gani wa Tanzania lakini macho ya watu wengi yanaonekana kuelekezwa kwa waimbaji wa Injili wa Kenya Bahati na Willy Paul ambao hivi karibuni walikuja Tanzania na kufikia kwenye studio za Wasafi ambazo zinamilikiwa na mwimbaji maarufu wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ambapo Mwimbaji Bahati ameshafanya kolabo na moja ya waimbaji kutoka kwenye lebo hiyo.
0 maoni:
Post a Comment