Jana ilikua ni siku ambayo Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Mfaume
amepumzishwa kwenye makazi yake ya milele. Rapa Nikki Mbishi amelezea
jinsi alivyokutana na msanii huyo.

Dogo Mfaume
Kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii, Nikki Mbishi amendika, “
Hereni
na Kazi ya Dukani ni classic hits za marehemu DogoMfaume. Nilikutana
naye Clouds Fm mwaka 2008 akiwa ameitwa na Ruge baada ya kufanya vizuri
sana na nyimbo zake.”
“
Nakumbuka Ruge hakumtambua Dogo Mfaume kwa haraka,
nilimsikia Dogo Mfaume akijitambulisha kwa Ruge “Mimi ni Dogo Mfaume,
nimepewa taarifa kuwa unahitaji nikuone”. Nakumbuka Ruge alivyostaajabu
“Ooh kumbe we ndo Dogo Mfaume, unafanya kazi nzuri sana” ila sikuweza
kujua kilichoendelea kwa maana mi nilienda kufuata mpunga wangu wa
mshindi wa Freestyle enzi hizo. All in all he was the great entertainer
kwenye fani ya uswazi,” Ameandika Nikki Mbishi.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment