Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amedai aliachana na
aliyekuwa mpenzi wake Harmonize miezi 3 iliyopita lakini waliamua
kuficha kwaajili ya shughuli zao za kibiashara.

Jacqueline Wolper
Muigizaji huyo ambaye alicheza vitendo kwenye video ya wimbo
‘Niambie’ wa Harmonize, amedai wakati kazi hiyo inatoka walikuwa tayari
wameachana lakini waliamua kushirikiana katika promo ya wimbo huo ambao
unafanya vizuri.
“Nyie mnajua sisi tumeachana juzi? Tumeacha miezi mitatu iliyopita
kabla hata ya wimbo wake Niambie haujatoka,” Wolper alikiambia kipindi
cha Shilawadu cha Clouds TV.
Aliongeza ,“Sisi wenyewe tuliamua kukaa kimya kwa sababu kuachana sio
kugombana kuna kesho mnaweza kushirikiana katika mambo mengine ya
kibiashara,”
Hata hivyo muigizaji huyo aligoma kueleza sababu ya kuachana na muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Happy Birthday’.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment