NSTAGRAM YATAJWA KUWA HATARI KWA WATUMIAJI

Instagram imeorodheshwa kuwa mtandao wa kijamii ambao una madhara zaidi kwa afya ya kiakili ya vijana.
Katika utafiti uliofanyiwa nchini Uingereza, vijana 1,479 wa miaka kati ya 14 na 24 waliombwa kueleza utathmini wao kuhusu mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kuzingatia wasiwasi, mfadhaiko, upweke, dhuluma na sifa za kimwili.
Instagram ndiyo iliyoongoza kwa kuwa na madhara zaidi. Instagram hujiuza kama jukwaa salama na la kusaidia vijana.
Mashirika ya hisani kuhusu afya ya kiakili yametoa wito kwa kampuni kuimarisha usalama wa watu wanaotumia mitandao ya kijamii.
Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Royal Society for Public Health unasema mitandao ya kijamii inafaa kutambua watu wanaotumia mitandao ya kijamii kwa kupitiliza na pia wale wenye matatizo ya kiakili.
Instagram husena huwa ina huduma na habari za kuwasaidia watu kukabili wanaotekeleza dhuluma na pia hutahadharisha watu kabla ya kutazama ujumbe, picha au video zenye madhara.
Inakadiriwa kwamba 90% ya vijana hutumia mitandao ya kijamii, na hivyo ndio huathirika zaidi.
Utafiti huo wa mtandaoni uliwauliza washiriki maswali kuhusu iwapo YouTube, Instagram, Snapchat, Facebook na Twitter zina madhara kuhusu afya yao na hali yao.
Washiriki walitakiwa waipe alama mitandao ya kijamii kuhusu masuala 14 ya afya na hali yao.
Kwa kufuata vipimo vyao, YouTube ilichukuliwa kuwa yenye manufaa mengi zaidi zaidi katika afya ya kiakili, ikifuatwa na Twitter na kisha Facebook.
Snapchat na Instagram zilikuwa na alama za chini kabisa kwa jumla.
Shirley Cramer, afisa mkuu mtendaji wa RSPH, alisema: "Inashangaza kuona Instagram na Snapchat zikiorodheshwa kuwa na madhara zaidi kwa afya ya kiakili na hali nzuri ya vijana - majukwaa haya mawili sana huangazia sura na sifa nzuri na mtu. Mitandao hii miwili inaonekana kuwafanya vijana wengi wajihisi kwamba hawatoshi au wana mapungufu fulani na hivyo kuwaongezea wasiwasi."

Wanachoshauri wataalamu:
  • Watu kutahadharishwa wanapokaa katika mtandao wa kijamii sana (vijana 70 waliohojiwa waliunga mkono hilo)
  • Wanaobainika kuwa na matatizo ya kiakili watambuliwe na waelekezwe kwenye majukwaa ambayo wanaweza kupata usaidizi
  • Mitandao ya kijamii kueleza picha ambazo zimehaririwa sana - mfano zinazotumiwa katika mauzo ya bidhaa, picha za wasanii na kadhalika. Mashirika ya matangazo yanaweza pia kutumia alama maalum kuonyesha picha zilizohaririwa sana kwa hiari.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment