Winga wa timu ya
vijana wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Abdul Suleiman aliyeibuka
mchezaji bora wa mechi ya Serengeti Boys na Angola hapo jana,
alichukuliwa na maafisaa wa CAF kufanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua
misuli.
Hali hiyo
ilisababisha ashindwe kwenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora hivyo
akawakilishwa na mlinzi, Dickson Job. CAF hawakuamini walichokiona kwa
Abdul ambaye alihaha uwanja mzima!
Hata hivyo baada ya vipimo ilibainika hakuwa katumia dawa hizo bali ni uwezo binafsi wa mchezaji uwanjani.
0 maoni:
Post a Comment