Polisi kuanza kukimbizana na magari ya wanafunzi!


 

 

 
Serikali mkoani Kilimanjaro imeagiza jeshi la polisi kufanya ukaguzi maalum wa magari yanayobeba wanafunzi ili kujiridhisha kama yana sifa ya kufanya kazi hiyo.
Mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecki Sadiki alisema hayo wakati wa Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) ambacho kilikuwa maalum kwa suala la hifadhi ya mazingira.
“Kikosi cha usalama barabarani kiandae mpango wa ukaguzi wa magari ya wanafunzi kila Jumamosi na yale yasiyo na sifa yaondolewe barabarani....hatuwezi kukaa kimya huku tunaendelea kupoteza maisha ya watoto wetu kama ilivyotokea mkoani Arusha” alisema.
Sadiki alisema Serikali ilisikitishwa na vifo vya watu wasio na hatia kwani pia katika ajali hiyo mkoa wake uliguswa kwa kupoteza watoto 14. Alimtaka Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamisi Issa kusimamia kikamilifu ukaguzi huo ili kuepuka udanganyifu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment