Rais wa Marekani Donald Trump
Kiwango
cha ukosefu wa ajira nchini Marekani kimepungua kwa kiwango kikubwa kwa
mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10 kufuatia kuimarisha
ujenzi wa ajira mwezi April , hatua ambayo inampa ahueni rais Donald
Trump baada ya kukabiliwa na takwimu mbaya za kiuchumi mapema katika
urais wake.
Baada ya kushuka
mwezi Machi, wakati ajira mpya zilishuka chini kutokana na dhoruba ya
majira ya baridi, idara ya uchumi wa Marekani iliongeza ajira mpya
zinazokadiriwa kufikia 211,000 huku kiwango cha ukosefu wa ajira
kikishuka mara kumi hadi asilimia 4.4, kiwango ambacho ni cha chini
zaidi tangu Mei 2007, wizara ya Kazi imearifu jana Ijumaa.
Ikulu ya White house imepongeza habari hizo baada ya robo ya kwanza wakati takwimu za uchumi zikionekana kuwekwa sawa na Rais Trump ameapa kuongeza ajira mpya milioni 25 katika kipindi cha mwongo mmoja jambo ambalo linakosolewa na wachumi kuwa halitawezekana.
Naibu msemaji wa ikulu Sarah Huckabee Sanders amesema idadi ya ajira inaonesha ajenda ya rais ya kupunguza kodi na kukuza uchumi wa Marekani.

0 maoni:
Post a Comment