Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto ambao wameidhinishwa na kuwania urais mwezi Agosti mwaka huu
Kenya State House
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameteuliwa na chama chake cha Jubilee, kuwania urais kwa muhula wa pili.
Uteuzi huu umetekelezwa na maelfu ya wajumbe wa chama hicho waliokutana jijini Nairobi hivi leo.
Hatua hii inakuja miezi michache kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe nane mwezi Agosti mwaka huu.
Akiwahotubia wajumbe wa chama chake, rais Kenyatta ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio ya serikali yake kwa muhula unaomalizika.
Amewasuta wanasiasa wa upinzani kama watu wasiokuwa na ajenda yeyote kwa wakenya na kuwaomba raia wa nchi hiyo kumchagua tena.
Hapo jana, chama kikuu cha upinzani cha ODM, kilimwidhinisha mwanasiasa mkongwe Raila Odinga kuwania urais kupitia muungano wa upinzani wa NASA.
Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema kutakuwa na ushindani mkali kati ya rais Kenyatta na Odinga ambao mwaka 2013 walipambana tena.
Kumekuwa na wito wa kufanyika kwa kampeni na uchaguzi wa amani nchini humo ili kuepusha machafuko ya baada ya uchaguzi kama ilivyoshuhudiwa mwaka 2008.
Kampeni rasmi inatarajiwa kuanza tarehe 30 mwezi huu.

0 maoni:
Post a Comment