Mkali wa muziki wa Hip Hop kutoka Morogoro, Stamina baada ya
jana kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Love Me’ aliomshirikisha Maua
Sama, leo hii aliripoti kuwa akauti yake ya YouTube kuibiwa lakini baada
ya saa moja ilirejea hewani.

Stamina
Stamina kupitia Instagram ameandika
‘Daah!, Bongo bwana
miyayusho sana, tukijitahidi hata kwa juhudi zetu kutafuta ugali wetu
kwa kutumia jasho letu na vipaji vyetu bado watu hawaoni. Wamehack
account yangu ya YouTube aisee!! nisipate viewers wengi? au ili
nisisonge mbele kimziki??? too sad ila sitokata tamaa mpaka mwisho wa
uhai wangu, mashabiki zangu samahani kwa usumbufu tatizo
linashughulikiwa nitawajulisha wataalamu wakimaliza kulisolve,”
aliandika Stamina kabla haijarejea.

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment