Ajali mbaya imetokea Karatu
Arusha katika mlima Rhotia baada ya basi dogo la St Lucky ya Arusha aina
ya Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi kutumbukia kwenye korongo na
kusadikiwa kusababisha vifo kwa wanafunzi kadhaa.
Basi la St Lucky ya Arusha ambalo lilikuwa limebeba wanafunzi waliokuwa wakienda kufanya mtihani wa ujirani mwema na wenzao Karatu likiwa limetumbukia kwenye Korongo.
Kamanda
wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kusema ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kuacha njia na
kuingia katika bonde la mto Mlera ambapo maiti wamepelekwa katika
Hospital ya Lutheran Karatu.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa kati ya maiti hizo miongoni mwao wapo waalimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wa kiume 11 na wasichana 18 nakufanya jumla yao kuwa maiti 32.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa kati ya maiti hizo miongoni mwao wapo waalimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wa kiume 11 na wasichana 18 nakufanya jumla yao kuwa maiti 32.
0 maoni:
Post a Comment